Friday 9 September 2016

DUUUHH WANAWAKE SHIDA

USITHUBUTU
*KUTIZAMA MPIRA UKIWA NA MWANAMKE NI
QUESTION QUESTION STRESS TUPU*
*Mke:* _Honey timu gani zinacheza leo?_
*Mume:* ```Arsenal vs Manchester Utd```
*Mke:* _oooh safi sana, ninaipenda Arsenal._
*Mume:* ```Safi hiyo timu nzuri sana, hujakosea
Darling.```
*Mke:* _Drogba anacheza?_
*Mume: ```Drogba hachezei timu
yoyote kati ya
hizi zinazocheza hapa.```
*Mke:* _Okey sweety. Oh huyo ni Chriss Brown?_
*Mume:* [akiwa ameboreka]
```Hapana huyo ni Theo Walcott.```
*Mke:* _Ahaa ila wanafanana sana. Hiyo kadi ya
njano aliyoonyeshwa huyo mchezaji n ya nin?_
*Mume:* ```Hilo ni onyo kwa mchezaji aliyeonesha
utovu wa nidhamu kwenye mchezo.```
_*```Baada ya dakika chache Wayne Rooney
akafunga gori la kwanza kwa Manchester utd```*_
*Mke:* [Huku akishangilia pasina kujua timu yake
ndiyo iliyofungwa]
_Oh oh Mume wangu Huyo ni walcot ndio
amefunga goli ee?_
*Mume:* [akiwa mpolee baada ya kufungwa]
```Hapana sio Walcott ni Rooney ndio ameifunga
Arsenal.```
*Mke:* [akiwa amefura hasira]
_Kwanini? Ilitakiwa Arsenal ndio ashinde._
*Mume:* [kimya]
*Mke:* _Hiyo kadi nyekundu aliyoonyeshwa huyo
mwenye kiduku ni ya nini?_
*Mume:* [akiwa ameboreka kweli kweli]
```Hiyo kadi nyekundu inamaanisha kwamba
mchezaji atoke nje kutokana na kufanya madhambi
uwanjani.```
*Mke:* _Kwaio akitoka nje anaenda kuwa kocha?_
*Mume:* [akiwa amechoshwa na maswali ya
mkewe huku akiwa hana utayari wa kujibu]
```Aaaaaaaa Hapana wife. Anatoka nje kabisa
hatakiwi kuonekana hata kwenye benchi la
ufundi.```
*Mke:* _kwaio kadi nyekundu ni kama taa za
barabarani._
*Njano=Onyo*
*Nyekundu=Hatari*
*Mume:* [akijibu tu ilimradi yaishe]
```Haswaaa mke wangu, hivyo hivyo.```
*Mke:* _Vipi kuhusu kadi ya kijani_
*Mume:* ```mmmmmh hapana kitu kama hicho
katika mpira wa miguu.```
*Mke:* _Nataka Arsenal ishinde kombe la Dunia_
*Mume:* [akaguna]
```Kombe la dunia ni mashindano ya mpira wa
miguu baina ya nchi na nchi na Arsenal sio nchi ni
klabu ya mpira. Inacheza kwenye ligi ya
Uingereza```
*Mke:* _Ni nani huyo mbaba aliyesimama amevaa
koti refu na anapua ndefu anaefanana na Mr.
Bean?_
*Mume:* [akiwa ameboreka haswa]
```Huyo ni kocha wa Arsenal anaitwa Arsene
Wenger.```
*Mke:* _Kwaio inamaanisha kwamba kocha wa
hiyo timu pinzani anaitwa Machester Wenger?_
*Mume:* [akabadilisha channel na kuweka *TBC1
kipindi cha chereko*

No comments:

Post a Comment